WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka rekodi ujenzi wa Mkongo wa Taifa , ambapo kwa mwaka mmoja pekee Wizara hiyo imefanikiwa kujenga kilometa 4442 za Mkongo wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew, alipotembelea Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida.
“Zamani wakati mkongo unaanza kujengwa, utekelezaji wake ulianza kutekelezwa na kampuni za nje, nakumbuka enzi hizo nikiwa mtaalamu katika utumishi wangu wa umma. Kulikuwa na kampuni ya CITCC wakati huo ambayo ndio ilitekeleza ujenzi huo kuanzia mwaka 2009 lakini mpaka kufikia mwaka 2016 tulikuwa tumeshajenga takribani kilometa 7,560”amesema Naibu Mhandisi Kundo.
Amesema kutokana na vijana wengi kusomea kazi hiyo na wataalamu wengi wa ndani ya nchi wakafanikiwa kujenga kilometa 350 na kampuni ya ndani ya nchi pamoja na kilometa nyingine 400 ambazo pia zimejengwa na kampuni ya ndani.