×

Darleen: Sijui Kama Bado Nipo Naye


MWANAMUZIKI Mwanahawa Abdul Juma almaarufu Queen Darleen amefunguka kuhusu ndoa yake na mfanyabiashara Isihaka Mtoro.

Queen Darleen ambaye ni dada mkubwa wa Diamond Platnumz, anakiri kuwa hana uhakika kama bado yuko kwenye ndoa au tayari ameachika.

Anasema kuwa bado anampenda mume wake na huwa wanawasiliana mara kwa mara “Kiukweli mpaka sasa sijijui. Sijui kama nipo kwenye ndoa au sipo kwenye ndoa Nampenda sana mume wangu, Popote alipo ajue kwamba nampenda sana. Yeye ndiye anajua kama nipo naye au sipo naye,” anasema Darleen kwa huzuni.

 

Kauli hiyo ya Darleen inakuja miezi kadhaa baada ya tetesi kuzagaa kuwa wanga wamepita na ndoa yake baada ya kujaliwa kupata mtoto mmoja na mfanyabiashara huyo

Stori: Sifael Paul

Leave a Comment