×

Harmonize Aitwa Mfalme Zumaridi

KWA alichokifanya bosi wa Lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize katika tamasha lake la Afro East Carnival pale Tabata[1]Shule jijini Dar, usiku wa kuamkia jana Jumapili, ilitosha kabisa kwa mashabiki wake kumpachika jina la Mfalme Zumaridi.

 

Kabla ya simulizi ya shoo yenyewe ambayo imeacha histori, ngoja nikujuze huyo Mfalme Zumaridi ni nani? Ukiacha simulizi za vita kati ya Urusi na Ukraine kisha kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, simulizi za Mfalme Zumaridi nazo zinashika kasi baada ya kutiwa  mbaroni na kufikishwa mahakamani jijini Mwanza kwa tuhuma za usafirishaji wa binadamu.

 

Kwa miaka kadhaa sasa, Mfalme Zumaridi ambaye jina lake halisi ni Diana Bundala, ni miongoni mwa wahubiri wa dini wanaovuma ndani na nje ya Jiji la Mwanza.

 

Mfalme Zumaridi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 39 ambaye hujiita Mungu wa Duniani, lakini la kushangaza ni kujiita Mfalme wakati ni mwanamke hivyo alitakiwa kujiita Malkia hivyo kuwa gumzo kwelikweli kiasi cha watu kuitana jina hilo kuonesha ubabe wa kile anachokuwa amekifanya mtu.

 

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Harmonize baada ya kufanya shoo ya kibabe mbele ya maelfu ya mashabiki wake jijini Dar huku akifanikiwa kukusanya wasanii wengi wakubwa ambao wengine ni ‘machawa’ wa aliyekuwa bosi wake kunako Lebo ya WCB, Diamond Platnumz.

 

Ukimuacha Harmonize, miongoni mwa wasanii waliofanya ‘wandaz’ na kupata shangwe la kutosha ni pamoja na Rich Mavoko, County Wizzy, Mr Blue, Snura, Matonya, Dulla Makabila, Amber Lulu, Gigy Money, Ben Pol, Marioo, Saraphina, Lord Music na wengine kibao.

 

Harmonize alifungua shoo yake hiyo alfajiri kabisa baada ya listi ndefu ya wasanii kupafomu huku akishushwa na lifti stejini akiwa na mtoto wake, Zuuh.

 

Kabla ya kuanza kushushwa zilipigwa fataki na baada ya hapo Harmonize alianza kushuka huku shangwe za mashabiki wa muziki zikipigwa kwa nguvu na hapo ndipo likaanza kusikika jina la Mfalme Zumaridi.

 

Baada ya hapo, huku akiwa na mtoto wake huyo stejini, kwa mara ya kwabnza alimuimbia kwa hisia wimbo wake mpya wa Bhakressa huku akisisitiza na kurudiarudia kwamba baada ya Rais anayefuata kwa ukubwa nchini Tanzania ni Bhakressa ambaye ni tajiri mkubwa Tanzania.

 

Akizungumzia mafanikio ya tamasha hilo, Harmonize au Konde Boy anasema kuwa, tiketi za kuhudhuria tamasha hilo ziliisha mapema hivyo kuwashukuru mashabiki wake na wadau wote waliomuunga mkono na kufanikisha jambo lake hilo.

Leave a Comment