×

Urusi Yashambulia Hospitali Tatu Ukraine

Rais wa Ukraine, Volodymir Zelensky

Hospitali ya wanawake wajawazito katika Mji wa Mariupol nchini Ukraine, Jumatano ya Machi 9, 2022 imepigwa makombora na majeshi ya Urusi ambapo inaelezwa kwamba watoto wachanga kadhaa wamefukiwa na kifusi.

Hayo yamesemwa na Rais wa Ukraine, Volodymir Zelensky kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter na kueleza kuwa huo ni ukatili wa kupitiliza unaofanywa na majeshi ya Urusi nchini humo, ambapo ameposti video inayoonesha baadhi ya majengo katika hospitali hiyo yakiwa yameharibiwa vibaya kutokana na shambulio hilo.
Video nyingine zinaonesha wagonjwa wakiwa wanajaribu kukimbia eneo hilo, wengi wakiwa wamejeruhiwa ambapo magari kadhaa pia yanaonekana yakiwa yamefukiwa na kifusi.

 

“Shambulio la moja kwa moja la majeshi ya Urusi katika hospitali ya wanawake wajawazito. Dunia itaendelea kuunga mkono ugaidi mpaka lini? Fungeni anga sasa hivi! Zuieni mauaji! Mnazo nguvu za kufanya hivyo lakini mnaonekana kupoteza utu,” ulisomeka ujumbe wa Rais Zelensky kupitia Twitter.

 

Mamlaka katika hospitali hiyo, zimesema imepata madhara makubwa ingawa hazikueleza ni watu wangapi waliouawa na waliojeruhiwa.

RIPOTI KAMILI: DADA ALIYENYONGWA NA MGANGA WA KIENYEJI, MFANYAKAZI WAKE AANIKA UKWELI ALIVYOWAAGA..

Leave a Comment