×

Mawazo mazito ya Diamond

 


HABARI ya mujini na anga za mitandao ya kijamii ni ngoma ya Nawaza ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond.”
Mashairi ya wimbo huo yamejaa mengi, lakini yafuatayo ni mawazo mazito kuwazwa na yeye pengine na binadamu wengine.

MOJA
Je, angekuwepo mzee Nyange (yaani marehemu baba yake) Uncle shamte angepata nafasi.
Sijui kama unaelewa anachowaza Diamond kwenye mashairi hayo? Chemsha bongo zako unaelewa jinsi ilivyo vigumu kumuwazia hivyo mama yako.

 

MBILI
Nawaza Vanny (Msanii wake Rayvanny kutoka Lebo ya WCB) na Elizabeth (Huyu kwa sasa ni mke wa mtu), clip zao zikivuja
Ndoa itaimarika eti, au ndio ataivunja.
Kwani kuna uwezekano wa kuwepo wa clip au ndo mawazo tu? Na mimi nawaza!

 

TATU
Ooh nawaza siku nikifa sijui wasafi itakufa, Nawaza sijui maradhi ama ajali itanikuta, Nawaza ooh, mama dangote nani chozi atamfuta?
Unafahamu kuwa sisi sote tutapita hapa duniani si ndiyo? Hebu waza pamoja na Diamond;
Mara paaap anaumwa kansa au kapata ajali kavunjika mgongo na hawezi kusimama itakuwaje mtaani?
Bila shaka haya ni mawazo mazito kwa sababu sisi ni viumbe na haya aliyowaza ni sehemu ya maisha yetu.

NNE
Ninachoshindwa kuoa kipi
Nikagundua naepusha lawama
Maana najijua kwa kucheat.
Hebu jiulize kwa nini Diamond haoi maana kama fedha anayo.
Wengine wanashindwa kuoa kwa sababu hawana uwezo, yeye anakwamishwa na nini?
Kuna penyenye zimekuwa zikipenyezwa kuwa kutokuoa kwake kunatokana na imani za kishirikina, lakini anapowaza yeye kinachomkwamisha ni kwamba yeye ni kicheche na fundi wa kupita mpango wa kando. Kazi kwenu kina dada!

TANO
Na nimejifunza binadamu kweli hawana jema
Yani mtoto unaemtunza ndio anakuombea ukilema, nashangaa.
Umeshawahi kusikia “tenda wema wende zako binadamu hawana shukrani eee!”
Basi ndiyo mawazo mazito anayowaza @diamondplatnumz kwamba kuna mtu unaweza kumhangaikia eeee… akitoboa tu anaanza visa na kukusagia kunguni kama siyo kukuombea ufe kabisa.
Toa maoni yako kuhusu ngoma ya Nawaza ya @diamondplatnumz

Richard Manyota

Leave a Comment