×

Kolabo ya Zuchu na Mondi Yaweka Rekodi

Kolabo pendwa na mashabiki wa msanii Diamond Platnumz na Zuchu iitwayo ‘Mtasubiri’ toka kwenye EP ya “First Of All” #FOA imefanikiwa kufikisha Views Milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya siku 9 pekee.

Wimbo huo umeweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza kufanya hivyo Afrika Mashariki. “Hii ndo Audio ya kwanza kufika 3,000,000 ndani ya siku 9 tu asanteni sana kwa mapenzi Mapokezi haya love yall” – Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ikumbukwe hii inakuwa ni kolabo ya TATU kwa Diamond na Zuchu, kolabo zao nyingine ni pamoja na ‘Cheche’ na ‘Litawachoma’.

Leave a Comment