
Serikali imesema itaendelea kushirikiana kampuni ya usambazaji mafuta ya Total Energies ili kuboresha sekta hiyo ya mafuta hapa nchini.
Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Waziri wa Nishati, Mhe January Makamba amesema serikali itaendelea kushirikiana na kampuni hiyo katika kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa kituo kikuu cha usambazaji mafuta hapa nchini.

‘”Mahitaji ya mafuta yameongezeka hasa kipindi cha janga la uviko 19 na kusabsbisha bei ya mafuta kuongezeka kutokana wimbi hili, serikali katika bunge lijalo tutajadili jinsi gani ya namna ya kutatua suala hili la upandaji mafuta”.Amesema Waziri Makamba.
Aidha Waziri Makamba ameongeza kuwa bei za mafuta zitazidi kupanda kutokana na vita vya Ukraine hivyo serikali itaendelea kuangalia ni namna gani ya upatikanaji wa nishati ya mafuta hapa nchini.
Amesema serikali inaipongeza kampuni hiyo kuzindua kituo cha solar ili kukabiliana na upungufu wa nishati katika sekta ya nishati hapa nchini.

Tunawapongeza Total kuzindua kituo cha solar total ni mdau wa uchumi wa maendeleoya katika nchi yetu”. Ameongeza waziri Makamba. Huku kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Total Energies, Jean Francois schoepp amesema lengo la kampuni hiyo nchini ni kuonesha mabadiliko na kuchochea sekta ya nishati hapa nchini ili wananchi kuendelea kupatiwa huduma zilizo bora kabisa.