×

Jamhuri Waweka Pingamizi Kesi ya Kutaka Makonda Ashtakiwe

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wajibu maombi katika kesi ya kutaka kibali cha kumfungulia kesi ya jinai aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda.
Akifafanua kuhusu mwenendo wa kesi  hiyo inayosikilizwa mbele ya hakimu mkazi  Aron Lyamuya  wakili wa upande wa waleta maombi Jerome Mwita Kicheere ameeleza kwa sasa mahakama inatarajiwa kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa na jamhuri kwa mjibu maombi namba moja na namba mbili ambao ni DPP na DCI.
Aidha naye Hekima Mwasipu wakili mwingine upande wa waleta maombi amebainisha kuwa upande wa mjibu maombi namba tatu ambaye ni Paul Makonda, wamewasilisha hati kinzani lakini hawajawasilisha pingamizi lolote.
Upande wa jamhuri umewasilisha Mapingamizi  manne ambapo moja kati ya hayo ni mahakama hii kutokuwa na uwezo wa kusikiliza maombi hayo.
Upande wa waleta maombi wakaomba mahakama ipange siku nyingine ya kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwa mahakamani na hivyo Hakimu Aron Ryamuya akaahirisha kesi hiyo hadi Aprili 8 mwaka huu.

Leave a Comment