
Walimu 25 kati 49 shule ya sekondari Sengerema iliyoko Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wameiomba Serikali kuwasaidia kukarabati nyumba zako za kuishi kutokana na uchakavu wa nyumba hizo hali inayopelekea kuhatarisha maisha yao kutokana na kuishi kwenye nyumba hizo.
Kauli hiyo imetolewa maarch 25 mwaka huu na Mkuu wa shule ya Sengerema Sekondari Zakari kahema wakati akisoma taarifa ya Shule hiyo kwenye sherehe za maafari ya 33 katika Shule hiyo.
Amesema Serikali kupitia Mamulaka ya elimu Tanzanaza TEA walikarabati miundombinu ya Shule 17 kongwe hapa nchini ikiwemo Sengerema Sekondari ambayo majengo yake yalikarabatiwa kwa Sh937milioni na kuyaweka katika mazingira mazuri hivyo basi wanaomba na kukarabati nyumba za walimu ili waweze kuishi katika mazingira bora.
Mwalimu Shedrack Kasomi nimiongoni mwa walimu 25 wa shule ya Sekondari Sengerema wanaoishi katika nyumba hizo amesema mazingira hayo wanayoshi siyo salama hivyo Serikali inatakiwa kuwaangalia kwa jicho la huruma kuwakarabatia nyumba hizo.
” Tangu mwaka 1972 Sengerema Sekondari ilipoanzishwa hadi leo mwaka 2022 miaka 50 sasa ambayo ni sawa na nusu karne nyumba hazijakarabatiwa Serikali ituangalie ” amesema Kasomi.
Sengerema Sekondari nimiongoni mwa shule 17 kongwe hapa nchini ambazo majengo yake yalikuwa yamechakaa kisha Serikali kupitia mamulaka ya elimu Tanzania TEA walikarabati miundombinu ya Shule hizo mwaka 2017/2018 na kuyafanya yawe katika hali nzuri.
” Hali za nyumba za walimu siyo nzuri naiomba Serikali itusaidie kukarabati nyumba hizo ili walimu waishi katika mazingira bora” amesema Kahema.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA ) Bahati Geuzye ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika mahafari ya 33 katika Shule hiyo amesema Serikali ya awamu ya sita itakarabati nyumba za walimu kwenye hizo shule kongwe ili walimu waishi katika mazingira bora.
“Ili mwalimu apate moli ya kufundisha na kuongeza ufaulu lazima waboreshewe mazingira ya makazi yake hivyo nimekubali ombi hilo tutalifanyia kazi na kulitekeleza ” Geuzye.
Jumla ya wanafunzi 576 kutoka taasisi 10 za Sayansi, Biashara na Saana wanatarajia kuhitimu masomo yako mwezi mei mwaka huu.
Katika suala la ufaulu kwenye shule hiyo Geuzye amewashukuru walimu kujitoa kwao na kuongeza ufaulu licha ya kuishi katika nyumba ambazo siyo bora wameonyesha uzalendo wao na suala la nyumba zao kufanyiwa marekebisho litatekelezwa.
Anastazia John ni mkazi wa Sengerema amesema walimu wanatakiwa kupata heshima ya kuishi katika mazingira bora kutokana na kazi wanazofanya za kufundisha watoto wetu .
Hivyo Mamlaka husika zinatakiwa kuwaonea huruma walimu wa shule ya Sekondari Sengerema kukarabati nyumba zao waishi katika Mazingira bora.
Mamlaka ya elimu Tanzania TEA amekubali kukarabati nyumba za walimu Shule ya Sekondari Sengerema ili kuwaondolea adha walimu wa shule hiyo wanaoishi kwenye nyumba chakavu.
STORI NA IDD MUMBA/ MWANZA