×

Klabu ya Yanga Yatinga Nusu Fainali Ya Kombe la FA Baada ya Kuichapa Geita kwa Penati

                                       Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Geita Gold FC

KLABU ya Soka ya Yanga imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama FA kwa kuifunga klabu ya Geita Gold FC kwa jumla ya mikwaju ya penati 7-6 baada ya mchezo kumalizika kwa kufungana bao 1-1.

 

Goli la Geita Gold FC lilifungwa na Paul Chikola katika dakika ya 87 na lile la Yanga likifungwa na beki wake Djuma Shabani kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 93 ya mchezo.

                         Mchezaji wa Yanga Jesus Moloko akiwa katika majukumu yake uwanjani

Katika mchezo Kocha Mkuu wa Yanga Nassredin Nabi alipewa kadi nyekundu kutokana na kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi na kwa maana hiyo anatarajiwa kukosekana katika pambano la Ligi Kuu dhidi ya watani wa jadi Klabu ya Simba.

Leave a Comment