×

Rais Samia Atuma Salamu Za Pole Kwa Rais Uhuru Kenyatta Kufuatia Kifo Mwai Kibaki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Rais Uhuru Kenyatta, wanafamilia na Wakenya wote kufuatia kifo Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki.

 

“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee wetu na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki. Afrika tumeondokewa na kiongozi mahiri na mtumishi bora wa umma. Nakupa pole kaka yangu Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta, wanafamilia na Wakenya wote. Mungu amweke mahali pema peponi. Amina.” amesema Rais Samia.

Leave a Comment