Mambo vepe wanangu wenyewe? Ndo kama hivo Saa Godi ametufikisha salama kwenye kukikata kitu cha mwaka so tunapaswa kumpigia saluti nini na nini ili kuonesha kumkubali kuwa ye ndo mpango mzima. Mpo hapo washkaji zangu wa ukweli? Kama vepe sogea kipande hii kwa jamvini hapa tukisanue arifu.
Nimekuwa na sistimu ya kuwasanua wana kuwa taimu inamuvu fasta kinoma na ukweli wa yestadei unaweza kuwa uongo wa tudei.
Sasa mazee si ndo tunaingia kwenye kitu cha mwaka niu brandi? Hapa sasa natoku na masela wangu wa kitaa. Wale tunaohaso pamoko na kutanua kwa mapene halali. Washkaji f’lani hivi ambao hatuna harufu ya ufisadi. Wale tunaosafa kinoma na hili laifu tukiwa apache alolo mifukoni hatuna kitu.
Achana na dili fekelo za magumashi. Unajua mtu fedenge ukiwa na ngawira au mawe ambayo umefaindi bila magumashi hata matumizi yake huwa hayana kabisa mastresi. Sasa wewe umetafuta mabovu dheni unatumbua kwa kujishtukia kwamba huenda kitanuka taimu yoyote si haina utamu mazee?
Ebana wanangu mmeshajaza dayari za mipango ya mwaka 2016? Yap! Huo ndo mpango mzima acha kupelekwa-pelekwa kama ling’ombe bila maplani. Kichwa timamu hakiendiendi tu bila madaireksheni.
Kuna wanangu walizijaza hizo dayari mwaka huu bati mambo hayakwenda freshi so mudi zipo dauni f’lani hivi bati wanachotakiwa kukinyaka ni kwamba hakuna matokeo ya mwisho yanayo-fanana katika kutafuta kuliwini hili laifu.
Kwenye haso zetu za deile kila kichwa kinajua kitawini vipi na kwa taimu gani. So usije ukakopi na kupesti kila kitu! Ni beta wanangu waka-sanuka kuwa kuwadi wa waifu wa maskini ni hazibendi wake! Sasa ili ueskepu kwenye situwesheni kama hizo ni masti uwe faita kinoma aisee arifu.
Wanangu jipangeni wala hakuna kukata tamaa kozi spidi yako tu ndo itakuchomoa mapema kwenye mwaka huu niu brandi. Weka silaha zako freshi kwa ajili ya 2016 ili neksti sizoni kama hivi tupeane marizalti tukiwa hepi. Oya cha msingi kachaa usikate tamaa kaza jombaa kitaeleweka tu. Ama nini machalii wangu.
Tudei hakuna ngendembwe. Ngoja nitumie chansi hii kuwapa sharauti wanangu wote fromu kila chobingo tuliokuwa hapa jamvini.
Ebana eee…nawawishi mwaka mpya wa 2016 wenye mafanikio kibwena. Kwa mizinguo kitaa usiache kunibonyezea kwenye foni hapo juu dheni unipe mastori moo nami nitayarusha kwa mahewa.
Tuwe pamoko tena neksti yia.