×

Drake Alamba Bingo, Asaini Mkataba Wenye Thamani ya Bilioni 928

Msanii Dris Drake amesaini mkataba na Universal Music Group wenye thamani ya Bilioni 928

DRAKE ni rapa wa kiwango cha Dunia wa Marekani ambaye anazidi kujipigia mkwanja tu kila kukicha.

Kwa mujibu wa akaunti ya Variety ya Twitter, Drake amesaini dili na Kampuni na Lebo ya Universal Music Group (UMG) ambalo linaripotiwa kuwa thamani yake ni shilingi bilioni 928 za Kitanzania.

Drake aliwahi kusainiwa na Lebo ya Cash Money kupitia Kampuni ya UMG Republic Records na sasa ametia saini tena kwa UMG kwa mkataba huo mpya.

Utajiri wa Drake unatajwa kufikia Dola za Kimarekani milioni 180.

Mkataba huo unaohusu kusimamia kazi zake za kurekodi, kuchapisha bidhaa pamoja na masuala ya video za muziki wake.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, utajiri wa Drake unatajwa kufikia Dola za Kimarekani milioni 180.
Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment