Rais Samia Afanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
Global Publishers May 5, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth) Mhe. Patricia Scotland mara baada ya kuwasili Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.
RAIS Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland Ikulu Tunguu Zanzibar, ambapo amekabidhiwa Azimio la Jumuiya ya Madola (Charter of the Commonwealth) kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Patricia Scotland mara baada ya mazungumzo yao leo Mei 05, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Azimio la Jumuiya ya Madola (Charter of the Commonwealth) kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Patricia Scotland mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.