
KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo, Ametoa Salam za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wa Mkoa Chama na Serikali baada ya kuwasili Ofisi za CCM mkoani Shinyanga kwa ziara yake ya Siku 9 katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu lengo likiwa ni kukagua utekelezaji wa mirada ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuimalisha na kuhimiza uhai wa Chama ngazi za mashina.
Akitoa salama hizo Katibu amesema kwasababu ya changamoto za kidunia baadhi ya bidhaa zimepanda bei kwahiyo Dunia nzima Imeathilika amesema Serikali imetengeneza njia ya kukabiliana na changamoto hizo.

Amesema lengo la Serikali nikupunguza mzigo kwa mwananchi,asijitokeze mtu yeyote kuwadanganya wananchi juu ya kupanda Kwa Bei ili kujitengenezea maslahi yake binafsi
Pia Ameongeza kwa kutoa rai kwa Viongozi wa Chama walio pewa dhamana kutenda haki kwa kufata taratibu za Katiba na sheria za Chama kuelekea kipindi cha Uchaguzi.