×

Mambo 10 Yaliyochangia Ubingwa wa Man City Premier 2021/22 …Soma Hapa

MANCHESTER City ilifanikiwa kutwaa taji la Premier League kwa msimu wa pili mfululizo wikiendi iliyopita chini ya Kocha Pep Guardiola.

 

Historia iliandikwa tena kwa Man City msimu huu wa 2021/22 na hii ni baada ya vita kali dhidi ya wapinzani wao Liverpool kwani bingwa wa Premier League alipatikana katika mchezo wa mwisho na timu hizo zikipishana kwa pointi moja tu.

 

Vita ilikuwa kali kwa Man City na Liverpool kwa mara nyingine msimu huu, mpaka City pale walipofanikiwa kutwaa taji hilo.

 

Hapa kuna mambo 10 ambayo yamechangiwa na taji hilo, lakini pia kuhusu msimu mzima ulivyokuwa.

City wameingia tano bora

Wakati Sheikh Mansour ameanza kuimiliki klabu hii mwaka 2008, Man City walikuwa wameshinda mataji mawili na la mwisho kushinda, ilikuwa ni mwaka 1968.

 

Lakini sasa tangu wamekuwa hapo wamefanikiwa kutwaa mataji sita ya Premier League na kufanya kufika nane na yale mawili ya nyuma. Kumbuka kuwa wenye mataji mengi ni Manchester United (20), Liverpool (19), Arsenal (13) na Everton (9) na wao wakifuata.

 

Mataji 10 ya ligi kwa Guardiola

Guardiola alipewa kazi ya kuhakikisha anatwaa mataji mara baada ya kutua kikosini hapo mwaka 2016.

 

Akiwa hapo kocha huyo amefanikiwa kutwaa mataji hayo sasa mara nne katika miaka sita ambayo amekuwa hapo, kumbuka akiwa Hispania aliweza kutwaa mataji matatu ya La Liga akiwa na Barcelona na akiwa Bundesliga pia alifanikiwa kutwaa mara tatu kwa maana hiyo kwa sasa ana jumla ya mataji 10 ambayo ametwa katika ligi tatu bora tofauti za Ulaya.

 

Walianguka na kuamka tena

Baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani wa Etihad, Man City walienda kucheza mechi 12 mfululizo bila kupoteza na kuweka gepu la pointi kwa Liverpool na wakiwa kileleni mwa msimamo.

 

Lakini mambo yalikuja kubadilika kwa Guardiola mara baada ya kupata kipigo kutoka kwa Southampton, Tottenhama na suluhu kutoka kwa Crystal Palace japo ambalo lilipunguza kasi yao dhidi ya wapinzani wao.

 

Sare ya 2-2 na Liverpool, mwezi Aprili mwaka huu na sare 1-1 dhidi ya Tottenham kwa Liverpool ndiyo kulisababisha City waweze kupumua na kuweza kufukuza na Liverpool vizuri katika kusaka ubingwa.

 

Vita nyingine na Liverpool

Ndiyo maana hata ligi ilipomalizika Man City walishinda kwa pointi 93 huku Liverpool wakiwa na pointi 92.

 

Msimu wa 2018/19, Man City walitwaa taji la Premier League wakiwa na pointi 98 wakipishana kwa alama moja na Liverpool ambao walikuwa na pointi 97 na msimu huu wa 2021/22 hilo limejirudia.

 

Ukuta wa Guardiola

Ubora wa safu ya ulinzi wa Man City ndiyo imekuwa chachu ya mafanikio yao kwa msimu huu na Aymeric Laporte akionekana kuwa bora zaidi kwani kiwango chake hakikuwa cha kubeza akiwa ameruhusu mabao 26 tu na ana clean sheet 21.

 

Wamefunga mabao mengi bila namba 9

Man City wamekuwa wakifunga mabao zaidi ya 100 kila msimu tangu Guardiola alipoanza kuwanoa mwaka 2016.

 

Wamekuwa bora kutokana na uwezo wa kufunga mabao mengi na kwa msimu wa 2021/22 Man City haikuwa na namba tisa halisi, lakini wachezaji 16 wa maeneo tofauti ndiyo waliweza kufunga mabao ndani ya kikosi chao.

 

De Bruyne, Rodri habari nyingine

Kevin De Bruyne na Rodri ambao ni viungo wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha Man City wanatwaa taji la Premier League kwa msimu huu.

 

De Bruyne amefunga mabao mara 15 na asisti nane, huku Rodri yeye akiwa ni kiungo bora hasa kwa msimu huu ambapo amefanikiwa kufunga mabao mara nane ndani ya Premier.

 

Grealish amefanya tofauti na matarajio

Katika usajili ambao uliwaangusha Man City basi ni huu wa Jack Grealish ambaye alitua kikosini hapo msimu huu akiwa amesajiliwa kwa pauni 100m.

 

Hakuwa na msimu bora Grealish licha ya usajili wake kuwa wa bei mbaya ambao uliandika historia ndani ya Premier League kwani amefunga mabao sita na asisti nne tu msimu huu ndani ya ligi.

 

City hawajabeba taji lingine zaidi ya Premier

Man City wamefurahia taji lao la Premier League likiwa ndiyo pekee ambalo wametwaa msimu huu.

 

City walipoteza mbele ya Liverpool katika nusu fainali ya FA na walipoteza Carabao Cup kwa penalti wakicheza dhidi ya West Ham United.

 

Lakini ulikuwa ni msimu mgumu kwao hasa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali baada ya kuondolewa na Real Madrid na ilikuwa baada ya kufanyiwa comeback ya nguvu na kuagaa mashindano hayo.

 

Haaland tumaini jipya

Mbeleni mambo yanaweza kuwa mazuri kwa Man City kutokana na ujio wa Erling Haaland ambaye atakuwa hapo msimu ujao.

 

Kwa msimu wa 2022/23, Guardiola atakuwa bora kwani atakuwa na namba tisa ingawa Haaland kama ataenda na mfumo na staili ya Premier League basi mambo yatakuwa bomba kwao.

MANCHESTER, England

MAYELE AITEKA SHOO Airport, YANGA WAKIWASILI kutoka MWANZA, MASHABIKI WAMVAMIA kwa SHANGWE..

Leave a Comment