×

Mwanajeshi wa Ukraine Ajitolea Kifo Ili Kuwaokoa Wenzake

 

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika ukaguzi wa maeneo ambayo mwanzo yalikuwa chini ya milki ya Urusi

Picha za video zimeonesha mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyeamua kujitoa mhanga ili kuwazuia wenzake wasishambuliwe na majeshi ya Urusi katika mji wa Novotoshkivske uliopo Jimbo la Luhansk ambapo kwa sasa kuna mapigano makali kati ya vikosi vya Ukraine na vile vya Urusi.

 

Baada ya askari mmoja wa Ukraine kushambuliwa na risasi na kupoteza maisha papo hapo ndipo majeshi yanayoiunga mkono Urusi yakaongeza mashambulizi na kulazimisha majeshi ya Ukraine kurudi nyuma kitendo kilichomfanya askari mmoja wa Ukraine kujitokeza mbele ya vikosi vya Urusi na kumimina risasi nyingi zilizosababisha wanajeshi yanayomuunga mono Urusi kurudi nyuma kwa muda, ingawa baada ya muda mfupi askari huyo aliuawa kwa kuzidiwa nguvu kwani yeye alikuwa pekeyake na wanajeshi wanaoiunga mkono Urusi walikuwa wengi.

 

Licha ya tukio lake hilo la kishujaa kuchukua uhai wake lakini aliwasadia askari wenzake kupata muda wa kurudi nyuma zaidi na kujipanga namna ya kukabiliana na mashambulizi ya vikosi vyenye mlengo wa Urusi.

 

Vikosi vya Urusi na Ukraine vipo katika mapambano makali kwenye miji ya Severodonetsk pamoja na Lysychansk ambayo kwa pamoja inakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 200,000 lakini pia ndiyo miji miwili pekee ndani ya Jimbo la Luhansk ambayo ipo chini ya milki ya vikosi vya Ukraine.

Wanajeshi wa Ukraine baada ya kurudi nyumba na kukwepa mashambulizi ya Urusi

Jimbo la Luhansk pamoja na Donetsk kwa pamoja inaunda Donbas, na majeshi ya Putin yamedhamiria kuishikilia miji yote ambayo haina raia wa Ukraine wanaounga mkono juhudi za Urusi katika kuishikilia miji hiyo.

 

Usiku wa kuamkia jana Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kuwa 90% ya majengo yote katika Mji wa Severodonetsk yameharibika na zaidi ya robo tatu ya makazi ya Jiji hilo yameshasambaratika kwani hakuna hata mawasiliano ya simu.

 

Meya wa Severodonetsk Oleksandr Striuk amesema zaidi ya raia 1,500 kati ya idadi ya watu 100,000 inayokadiriwa kuwemo ndani ya Jimbo lake tayari wameshafariki kutokana na mapigano lakini pia kutokana na kukosa dawa kwasababu ya magonjwa yasiyotibika.

Leave a Comment