×

Rais Samia Atoa Onyo kwa Watanzania Watakaokwenda Kufanya Biashara Haramu Nchini Qatar

Rais Samia aiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa soka akiwemo mjumbe wa FIFA kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Juliano Beletti

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa watanzania wanaofikiria kwenda kufanya huduma haramu nchini Qatar wakati wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini humo.

 

Rais Samia amesema wataokwenda kutoa huduma haramu nchini Qatar watakamatwa, ameyasema hayo wakati anakabidhiwa Kombe la Dunia ambalo limeletwa nchini chini ya mjumbe wa FIFA ambaye ni mchezaji wa zamani wa Klabu ya Barcelona, Chelsea na Timu ya Taifa ya Brazil Juliano Beletti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Kombe la Dunia

Kwa upande mwingine Rais Samia ametoa maagizo kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri wake Mohamed Mchengerwa kuangalia fursa mbalimbali ambazo Watanzania wanaweza kuzitumia katika kujipatia kipato kutokana na mashindano hayo ya Kombe la Dunia nchiniQatar lakini pia fursa ya kutangaza vivutio vya utalii pamoja na uwekezaji.

Leave a Comment