×

Rais Samia Afungua Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Makatibu Mahsusi(PICHA+VIDEO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa Mwaka wa Makatibu Mahsusi kutoka mikoa mbalimbali nchini, mkutano ambao umefanyika Jijini Dodoma.

 

Katika Hotuba yake Rais Samia amewaasa Makatibu Mahsusi kuwa waadilifu na wenye weledi katika maeneo wanayofanyia kazi, pia amesisitiza kuwa wenye kuchapa kazi na kujiheshimu ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu watu wengine.

Makatibu Mahsusi wakiwa katika mkutano wa mwaka uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa rai kwa Makatibu hao kuhakikisha wanajiendeleza katika masomo yao lakini pia katika dhana nzima ya utendaji kazi bora na kwa wakati kwani hicho ndiyo kitu pekee kinachowafanya waitwe Makatibu Mahsusi.

 

“Napiga Mstari kwenye uweledi na uadilifu, katibu mahsusi lazima awe mwenye uweledi na muadilifu, unapokosa uadilifu unabaki kuwa mpiga chapa tu.”

Rais Samia amehimiza uadilifu na weledi wa kazi kwa Makatibu Mahsusi

Rais amesisitiza Makatibu Mahsusi kuweka na kutunza siri za wakuu wao kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza tija katika kazi zao lakini pia kunaboresha mazingira ya kazi, Rais pia amebainisha kuwa Makatibu Mahsusi wanamchango mkubwa sana kwa wakuu wao kwenye mazingira yao ya kazi kwani wao ndiyo wanaowafanya wakuu wa idara na ofisi mbalimbali kufanya kazi kwa ufanisi.

Leave a Comment