×

Vodacom Tanzania Yashirikiana na Samaki Samaki Kuwazawadia Wateja

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa akikabidhiana mkataba na Mwenyekiti wa migahawa ya Samaki Samaki, Carlos Mella (Kalito) wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Vodacom na migahawa hiyo itakayotoa zawadi kwa wateja wa Vodacom watakaolipia kwa kutumia M-Pesa watarudishiwa asilimia 10 ya malipo yao na pia wateja wote watapata huduma ya bure ya WiFi.

 

 

Dar es Salaam, 3 Juni 2022. Vodacom Tanzania Plc, kampuni inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini, imefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa Habari na Mgahawa wa Samaki Samaki uliofanyika kwenye mgahawa wao uliopo Masaki na kutangaza ushirikiano wao.

Ubia huo mpya unalenga kuwawezesha na kuwazawadia watumiaji wa Vodacom wanaotembelea migahawa ya Samaki Samaki na kutumia mfumo wa Vodacom wa M-Pesa Kufanya malipo.

Walivyosainishana mikataba

 

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa alisema, “Tunafurahia sana kushirikiana na Samaki Samaki, jina ambalo limejizolea wapenzi wakweli miongoni mwa wateja wake., kama vile ilivyo kwetu sisi Vodacom Tanzania. Kwa hiyo ni vema kabisa kwetu sisi kushirikiana kuwapatia wateja wetu huduma bora na kuwazawadia uamiinfu wao kwetu.”

Samaki Samaki walianza na tawi moja tu mjini Dar es Salaam ambalo  liliwapatia umaarufu haraka na kupelekea kuanzishwa kwa tawi lao la pili huko Masaki. Migahawa hiyo hutoa vyakula safi vya baharini, katika mandhari bora zaidi na kuwapatia wateja huduma bora mgahawani kwa bei nafuu.

Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo.

 

 

Kwa ushirikiano huu mpya, unaolenga kuwahusisha zaidi vijana, watumiaji wa Vodacom wanaotembelea Samaki Samaki wataweza kutumia mtandao wa kasi ya juu wa Vodacom 4G kupitia Wi-Fi bila malipo kwenye migahawa hiyo. Zaidi ya hayo, wale wanaolipa kupitia M-Pesa watarejeshewa 10% ya pesa taslimu kwenye vyakula na vinywaji vyao.

Vodacom inatumia fursa hii kuendeleza kampeni ya kutumia malipo ya kidijitali kwa matumizi ya kila siku. Malipo ya kidijitali ni salama kwa wafanyabiashara kwani wanalinda mtaji kutokana na hatari za wizi au upoteajina vile vile humuondolea mlipaji adha ya kutafuta ATM, kupanga foleni kwenye benki, kutafuta chenji au kubeba pesa taslimu itakayohitajika kwa miamala yake.

Kwa wageni wanaotembelea migahawa hiyo siku za Jumamosi, kutakuwa na matukio mbalimbali ya uhamasishaji ili kuzalisha ushirikiano na kutakuwa na shughuli nyingi za kusisimua na za kuburudisha.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mwenyekiti wa Samaki Samaki, Carlos Mella  alisema, “Ushirikiano huu umekuja wakati muafaka, kwa kuwa tumejenga wateja waaminifu wanaofurahia huduma zetu kuu na tunajua tukiwa na mfumo wa M-Pesa, tutaweza kupunguza adha za malipo kwa wateja wetu wakiwa kwetu. Pia tunatazamia shughuli nyingi tulizopanga kwa watumiaji wa Vodacom kwenye migahawa yetu. Nyote mtafurahi!”

Ushirikiano huu mpya unaendana na mkakati wa Vodacom Tanzania wa kuongeza uelewa wa chapa na ushirikishwaji wa wateja ili kuwazawadia watumiaji wa huduma zake.

Kuhusu Vodacom Tanzania PLC

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya huduma za mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi wa data nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa watumiaji zaidi ya milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni zake ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inamilikiwa na Vodafone Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA

Kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.vodacom.co.tz

Leave a Comment