
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) leo imetoa tahadhari ya upepo mkali unaotarajiwa kutokea kwenye siku tano zijazo katika maeneo ya ukanda wa Pwani ya bahari ya Hindi ambayo ni Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es salaam na Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Taarifa ya Mamlaka hii imesema hii ni tahadhari ya upepo mkali unaofikia kilomita 50 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 3 ambapo athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuathirika kwa shughuli za uvuvi na usafirishaji baharini, nyumba zenye mapaa yasiyo imara kuezuliwa, vumbi kupeperushwa na kupunguza uono n.k
Angalizo jingine kwenye taarifa ya TMA June 2 2022 limesema kunatarajiwa upepo mkali unaofikia kilometa 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Mwnaza, Mara, Kagera, Geita, Mwanza na Simiyu), Ziwa Nyasa (Mikoa ya Ruvuma na Njombe), pamoja na kusini mwa Ziwa Tanganyika (Mikoa ya Katavi na Rukwa).
