×

Kidato cha Tano na Sita Kusoma Bure, Kupunguza Gharama kwa Wazazi, Walezi -Video

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

 

Serikali imependekeza kufuta rasmi ada katika elimu ya ngazi ya kidato cha tano na sita ili kuwapunguzia gharama za kusomesha wazazi, walezi ikiwa ni sambamba na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi ya elimu bure.

Akitangaza Bungeni jijini Dodoma wakati wa uwasilishwaji wa Bajeti Kuu, leo Juni 14, 2022 Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata haki ya elimu.

Mwigulu ameongeza kusema kuwa jumla ya wanafunzi wa kidato cha tano nchini ni takribani milioni 60, huku wale wa kidato cha sita wakiwa ni milioni 55 hivyo kufanya gharama za ada kuwa Tsh. bilioni 10 kwa mwaka gharama ambayo Serikali inaimudu.

“Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza Wizara, napendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

“Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita. Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa. Nani kama SAMIA? Nani kama Mama? Nani kama CCM? CCM ni Na. 1,” amesema Mwigulu.

Hatua hii inapelekea elimu kuwa bure kuanzia ngazi ya msingi yaani darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

BAJETI KUU – DENI LA TAIFA LAONGEZEKA, SERIKALI YAFUTA ADA FORM 5 na 6, MWIGULU ANAWASILISHA

Leave a Comment