
LEO tarehe 14 Juni 2022, Mhe. Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar ambaye ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 12 wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Daren Tang, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (WIPO).

Waziri amemshukuru Mkurugenzi Mkuu huyo kwa miradi na programu zilizotekelezwa na shirika hilo nchini.
Kwa upande wake Bw. Tang ameahidi kutekeleza miradi/programu zaidi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo ya kilimo, ubunifu, kuandaa sera ya Haki Miliki, kuwajengea uwezo wajasiliamali vijana na wanawake.
Aidha, ameahidi kuwajengea uwezo wataalam wanaosimamia masuala ya Hakimiliki na Mahakama ya Biashara.