×

Azam Yamtambulisha Sopu kama Usajili Mpya, Simba na Yanga Zatajwa Kuambulia Manyoya

Sopu amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia Azam FC

KLABU ya Azam imemtambulisha kiungo mshambuliaji Abdul Seleman Sopu kama mchezaji wao mpya akitokea Coastal Union ya Tanga.

Sopu ndiye mfungaji bora wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup

Sopu ambaye ndiye mfungaji bora wa michuano ya Azam Sports Federation Cup iliyomalizaka mwishoni mwa juma akiwa na magoli 9, akifanikiwa kuweka rekodi ya kufunga magoli matatu (Hat Trick) kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo, waliyocheza dhidi ya Yanga

Amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia wanalambalamba Azam Fc.

Kabla ya kujiunga na Coastal Union, Sopu alihudumu katika klabu ya Simba

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ni kwamba mchezaji huyo alikuwa akihusishwa na vilabu vya Kariakoo vya Simba na Yanga lakini ni Azam FC ndiyo walioibuka kidedea kwa kuinasa saini ya kinda huyo ambaye alipita pia katika klabu ya Simba kabla ya kutimkia kwa Wanamangushi Coastal Union.

Leave a Comment