×

Eriksen Akubali Kujiunga na Manchester United, Asubiri Kufanyiwa Vipimo vya Afya

Christian Eriksen kiungo wa Brenford na Timu ya Taifa ya Denmark

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Brentford ya nchini Uingereza Christian Eriksen amekubali kujiunga na miamba ya soka nchini Uingereza klabu ya Manchester United kwa mkataba wa miaka 3.

Kocha mpya wa Manchester United Erik Ten Hag

Eriksen (30) aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama vile Ajax Amsterdam, Totenham Hotspurs, Inter Milan pamoja na Brentford ameonesha nia hiyo ikiwa ni sehemu ya ndoto yake ya kufanya kazi na kocha mpya wa sasa wa Manchester United raia wa Uholanzi Erik Ten Hag.

Kiungo wa Brentford Christian Eriksen

Msimu uliopita kiungo huyo alilazimika kucheza kwa mkopo katika klabu ya Brentford baada kupona kutokana na shambulio la moyo alilolipata katika mashindano ya Euro 2020 yaliyofanyika mwaka jana.

 

Nyota huyo anayeiwakilisha Timu ya Taifa ya Denmark amekuwa katika kiwango kizuri na kuiwezesha klabu ya Brenford kubaki Ligi Kuu ya Uingereza.

 

 

Leave a Comment