Msanii Faustina Mfinanga almaarufu kama ‘Nandy’ amejikuta akitokwa na machozi ya furaha madhabahuni wakati akila kiapo cha ndoa leo Julai 16, 2022 ambapo amefunga pingu za maisha na msanii William Lyimo maarifu kama Billnass.
Ndoa hiyo imefungwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach Dar es salaam.