
Kwa miaka mingi, pamekuwa na mjadala wa mara kwa mara juu ya utendaji kazi usioridhisha wa kampuni binafsi ya Kimataifa ya kuhudumia makontena Tanzania (Tanzania International containers Terminal Service- TICTS). Sehemu kubwa ya mjadala umewahusisha wadau wa biashara, viongozi wa Serikali, wabunge na wataalamu.
Hivi karibuni wadau wa biashara wametoa mapendekezo yao wakiisihi Serikali kutokuipa mkataba mpya kampuni hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake mwaka huu. Pia, Waziri Mkuu Ndugu Kassim Majaliwa mwezi April mwaka huu alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa agizo kwa kampuni hiyo kuimarisha utendaji kazi wake ili kuondoa kero ya ucheleweshaji wa mizogo katika Bandari ya Dar es Salaam.
