
GOOD news kwa wapenzi wa movie ni kwamba sehemu ya pili ya movie iliyopata mafanikio makubwa duniani na kupendwa na watu wengi BlackPanther: Wakanda Forever, inatarajiwa kuachiwa rasmi Novemba 11, 2022.
Tayari official trailer yake huku yenyewe BlackPanther: Wakanda Forever imeshaachiwa kwenye platforms za movies duniani huku ikitarajiwa kufanya mauzo makubwa na kuipiku ile ya awali.

Sehemu hii ya pili ya BlackPanther: Wakanda Forever inaachiwa bila uwepo wa mfalme wa Movies hiyo, Chadwick Boseman (Black Panther) aliyefariki dunia mnamo Agosti 28, 2020 akiwa na miaka 43 jijini Los Angeles nchini Marekani kwa matatizo ya saratani ya utumbo mpana.
Chadwick alijipatia umaarufu mkubwa kwenye filamu ya “Black Panther” kutoka studio za Marvel akiigiza kama Mfalme T’Challa.
Filamu ya Black Panther ni moja ya filamu pendwa zaidi duniani kwa namna wahusika wake walivyo wa kipekee na waliobeba asili na tamaduni za Kiafrika ba inatengenezwa na kampuni ya Disney inayoshirikiana na kampuni ya Marvel.

Black Panther kwa mara ya kwanza ilioneshwa rasmi, Januari 29, mwaka 2018 huku ikiwa na mastaa kibao wenye asili ya Afrika na Marekani; Chadwick Boseman, Lupita Nyongo wa Kenya, Michael B. Jordan, Martin Freeman na wengineo.
Filamu zingine ni kama; The Marvel ambayo itatoka Februari 2023 huku Ant-Man ikitarajiwa pia kutoka Julai 2023.