
WANASAYANSI walisema maambukizi ya magonjwa kati ya wanyama wa kufugwa kama vile paka na mbwa kutoka binadamu hayajawahi kuripotiwa mpaka siku za hivi karibuni ambapo mbwa aina ya “greyhound” ambae alikuwa akilala kitanda kimoja na wamiliki wake nyumbani kwao Ufaransa aliporipotiwa kuugua ugonjwa wa “Monkeypox”. Wanasayansi hao wanatoa wito kwa wananchi juu ya hitaji la kuwatenga wanyama kutoka kwa watu walio na “Monkeypox”.
Wamiliki wa mbwa huyo walikwenda hospitali mjini Paris tarehe 10 Juni baada ya kupata vidonda. Chini ya wiki mbili baadaye, mbwa wao alionyesha dalili kama vile vidonda kwenye tumbo lake kabla ya kuthibitishwa na watafiti katika Chuo Kikuu cha Sorbonne kwamba pia alikuwa na “Monkeypox”.

“Matokeo yetu yanapaswa kuibua mjadala juu ya hitaji la kuwatenga wanyama kutoka kwa watu walio na virusi vya monkeypox,” watafiti waliandika katika ripoti hiyo,tunatoa wito kwa uchunguzi zaidi juu ya maambukizi kupitia wanyama .

Monkeypox imeambukiza karibu watu 1,700 nchini Ufaransa huku kesi zaidi ya nchi 80 zikiripoti hadi mwisho wa juma lililopita.
Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao