
BEIJING Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko jimbo la Qinghai kaskazini mwa nchi ya China yamesababisha vifo vya watu 16 huku wengine 36 wakiwa hawafahamiki walipo.
Mvua hiyo kubwa na ya ghafla ilianza kunyesha siku ya jumatano jioni maeneo ya milimani mwa jimbo hilo la Qinghai na hivyo kusababisha mmomonyoko wa ardhi na mikondo mikubwa ya maji kuelekea maeneo ya makazi ya watu.

Mito ilifurika kwa maji na kubadilisha njia kuelekea maeneo ya vijiji na miji. Zaidi ya watu 6200 wameathiriwa na mafuriko hayo.

Serikali imefanya jitihada za uokoaji kwa kutuma timu ya watu zaidi ya 2000 na magari 160 kusaidia zoezi hilo la uokoaji.
Imeandikwa: Simon J. Molanga kwa msaada wa mitandao