
KLABU ya Chelsea pamoja na Totenham Hotspurs zote za nchini Uingereza zinapigana vikumbo kuwania Saini ya kinda wa Everton Anthony Gordon.
Tayari Cheslea imeshatuma ofa mbili ambazo zote zimekataliwa huku msimamo wa Everton ukiwa ni kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Gordon (21) ni kinda aliyepandishwa timu ya wakubwa kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo na taarifa zinadai kuwa Chelsea ipo tayari kutoa hadi kitita cha Paundi milioni 60 ili kuinasa Saini ya kinda huyo.
Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel anasemekana kuwa ndiye anayeshinikiza usajili huo kukamilika kwa haraka kwani anamuona kinda huyo kama mbadala sahihi wa winga Hakim Ziyech anayetarajia kutimkia katika klabu yake ya zamani ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi.

Aidha kocha wa Totenham Hotspurs muitaliano Antonio Conte ameushinikiza uongozi wa klabu hiyo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha inapambana na Chelsea ili iweze kuipiku timu hiyo kwenye usajili wa Gordon.