×

Fahamu ni Jinsi Gani Unaweza Kuimarisha Kumbukumbu Yako

Utunzaji wa kumbukumbu una mambo kadhaa ya kuzingatia

KUPOTEZA kumbukumbu kwa mwanadamu ni hali ya kawaida ambayo kitaalam inajulikana kama “Amnesia”

Wakati mwengine kupoteza kumbukumbu kukizidi inakua ugonjwa kwa kitaalam unajulikana kama “Dementia”

Mara nyingi kupoteza kumbukumbu kunatokea pale ambapo mtu kutokua na umakini pindi anapo fatilia au kusikiliza jambo anesema Profesa Richard Restak, wa Chuo Kikuu cha George Washington Marekani.

 

Jinsi ya kuimarisha kumbu kumbu

Epuka vilevi.

Vilevi ni hatari kwa afya ya ubongo. Vitu vyovyote vinavyo athili ufahamu wa ubongo au kusababisha kupoteza fahamu vinapaswa kuepukika ili kuimarisha kumbukumbu yako.

Kulala usingizi nako kunasaidia kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu

Lala usingizi wakutosha.

Kulala kidogo mchana kunasaidia kuongeza kumbukumbu na kukaa macho kwa muda mrefu kunadhoofisha utendaji kazi wa ubongo hivyo kudhoofisha kumbukumbu.

 

Kuchangamana na watu.

Kuchangamana na kuwa na watu inasaidia kupunguza hali ya upweke hivyo kuimarisha kumbukumbu.

Profesa Richard Restak anasema kwakufuata mambo yote haya hakuta kuhakikishia kuwa na kumbukumbu nzuri ila kwakufata ushahuri huu utasaidia kupunguza athari za kupoteza kumbukumbu.

 

Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mtandao.

Leave a Comment