×

Nini Kitatokea Baada ya Vita Kufikisha Nusu Mwaka Kati ya Ukraine na Urusi

Madhara yatokanayo na vita kati ya Urusi na Ukraine

WATAALAMU wanasema Ukraine inahitaji kufanya maendeleo kusini-magharibi mwa nchi wakati wa msimu wa baridi kali na jinsi Vladimir Putin anaweza kujaribu kutaka ushindi kwa Urusi.

 

Nusu ya mwaka wa vita hivyo inaendana na Siku ya Uhuru wa Ukraine, ambayo katika hali ya kawaida ingeshuhudia raia wakisherehekea miaka 31 ya uhuru kutoka kwa Umoja wa Kisovieti wa zamani.

Vikosi vya Urusi

Katika hali ambayo inatia hofu kwa Ukraine ni ile kinachodaiwa na Urusi kuwa Ukraine imehusika na mauaji ya wanajeshi wake hiyo inapelekea Ukraine kuhisi Urusi inaweza kufanya mashambulio dhidi ya raia wake na kulenga sehemu muhimu kwa jamii.

Vikosi vya Ukraine

Lakini ushindi wa Ukraine unategemea mambo mengi muhimu, ikiwa ni pamoja na muda ambao nchi za Magharibi zimejitayarisha kutoa msaada na kama wanajeshi wanaweza kupata mafanikio ya kutosha kabla ya majira ya baridi kuanza.

 

Hapa tunaangalia kile tunaweza kutarajia kuona ardhini huko Ukraine na kutoka Kremlin katika miezi ijayo.

 

Imeandikwa:Leokadia Chaarles kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment