×

Video: Kesi ya Uchaguzi wa Rais Kenya: ‘Ruto Hakupata Asilimia 50+1 ya Kura’-Wakili wa Odinga, James Orengo

KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya leo Agosti 31, 2022 inaendelea huku majaji wa mahakama ya Juu zaidi wakisikiliza ushahidi na mawasilisho ya upande wa mgombeaji wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

 

Wakili wa Raila ,James Orengo amewasilisha stakabadhi za ushahidi kuonyesha kwamba William Ruto aliyetangazwa kuwa mshindi hakupata asilimia 50+1 ya kura zilizopigwa.

 

Orengo amedai kwamba kulikuwa na tofauti ya idadi ya wapiga kura ambao mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati alitangaza kwamba walijitokeza kupiga kura.

 

Mawakili wa Odinga pia wamedai kwamba kulikuwa na visa vya kura kuondolewa kutoka kwa Raila na kuongezwa kwa zile za mpinzani wake Ruto ili kuhakikisha kwamba anaafikia kiasi cha idadi ya kura zinazohitajika ili kutangazwa mshindi.

Leave a Comment