
KUTANA na kijana Ben Yu kutoka nchi ya marekani mwenye miaka 26, Ben Yu aliakuwa akisoma katika chuo cha Harvard, aliamua kuacha chuo na kuanza kucheza Bitcoin baada ya muhula mmoja wa masomo na hapo ndipo historia ya utajiri wake ulipoanzia.
Licha ya utajiri wake lakini kilicho washangaza wengi kijana Ben Yu yeye huishi kwenye gari lake ambalo linaitwa Rv van na mara nyingi wezi humuibia gari lake lakini huwakamata kwa kuwa amefunga mfumo wa kuonesha mizunguko ya gari hilo.
Mara tu baada ya kutajirika kijana Ben Yu alijiwekea ahadi kuwapa pesa kama msaada watu wasio na makazi lakini pia aliweka ahadi ya kuwanunulia magari ambayo watayatumia kama nyumba ili wawe majirani zake.