×

Wabunge Kulipwa Mishahara Mikubwa DRC Congo Yazua Taharuki

Martin Fayulu

WABUNGE wa DRC Congo wamezua taharuki kwa wananchi wao kwa kulipwa mishahara mikubwa karibuni dola 21,000 kwa mwezi bila kujali kuwa kongo ni moja kati ya nchi masikini zaidi duniani,kitendo hicho kimeibua hasira kwa wananchi wa Congo siku ya juma tano, malalamiko hayo yalikuwa ni ya  kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

kiongozi wa upinzani Martin Fayulu alisema uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa  juu ya swala hilo ili kujua kiwango ambacho wabunge wa Congo wanapokea kila mwezi.

 

Samuel Mbemba

Samuel Mbemba mbunge anae fanya kazi na spika wa bunga amekanusha taarifa hizo zilizo ibua  taharuki na sintofahamu katika nchi ya Congo na kusema kwamba Martin Fayulu  alikuwa “anaota” kutoa manung’uniko hayo.

 

Tresor Kibangula ambae ni mchambuzi kwenye taasisi ya utafiti ijulikanayo kwa jina la Ebuteli anakadiria kuwa kiwango hicho cha mshahara wa wabunge ni sahihi.

 

Imeandikwa: Leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment