×

Wakili wa Raila Aonyesha Fomu Katika Seva ya IEBC Ilio na Jina la Raia wa Venezuela -Video

Wakili wa Raila aonyesha fomu katika seva ya IEBC ilio na jina la raia wa Venezuela

Wakili wa Raila Odinga katika kesi anayopinga uchaguzi wa Rais Mteule William Ruto katika mahakama ya Juu Julie Soweto alionyesha moja kwa moja kanda ya video ilioonesha hitilafu kutoka kwa tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC.

 

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga uchaguzi wa urais, alitoa fomu katika tovuti hiyo kutoka Shule ya Msingi ya Gacharaigo katika Kaunti ya Murang’a iliyokuwa na jina la raia wa Venezuela Jose Camargo.

 

“Mahali nilipo muhuri wa IEBC unaonekana umepachikwa juu ya muhuri mwingine. Tumeombwa tuonyeshe jinsi takwimu zinavyobadilishwa. Tukiangalia kura zilizopigwa, nambari ya kwanza ni ya Raila Odinga aliyepata 55, Ruto 260 , Mwaure 1 na Wajackoyah 0.

 

Iwapo tutajumlisha jumla ya kura zilizopigwatunapata 316. Jumla ya kura zote zilizopigwa katika fomu hii ni 321, ikiwa ni tofauti na kile tulichoona. Hii ikimaanisha kwamba tayari hesabu hiyo ina makosa’’, alisema

 

‘’Tuliambiwa na bwana Eric Gumbo wakili wa IEBC kwamba hakukuwepo raia wa kigeni katika uchaguzi huu. Tuliambiwa kwamba hawakuweza kuingilia seva za IEBC . Tazama Juu kushoto katika fomu hii kuna jina la Jose Camargo. Huyu ndiye mtu aliyefanya maamuzi ya uchaguzi huu. Je jina hili liliingiaje hapa?’’ , aliuliza

 

Bi Soweto alihoji kwamba bwana Carmago ndiye aliyekuwa akiingilia fomu zote 34ª katika seva ya tume ya Uchaguzi ya IEBC.

 

‘’Ishara ya kuingilia fomu hizi iliwachwa. Kwa Neema ya Mungu , tulipata kitu . Hili hatukujifanyia. Hivi ndivyo mambo yalivyofanyika’’

Leave a Comment