×

Kocha wa Yanga Awapangulia Kikosi Zalan FC Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Mkapa

KUELEKEA katika mchezo kati ya Yanga dhidi ya Zalan FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi amesema kuwa watu watarajie kuona mabadiliko katika kikosi chake tofauti na kile ambacho kimeanza katika mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Azam FC.

 

Katika mchezo huo ambao Yanga walitoka sare ya mabao 2-2 kocha Nabi alifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji kama Djuma Shabani na nafasi yake kutumiwa na Dickson Job huku Joyce Lomalisa akicheza beki wa kushoto.

Wachezaji wa Yanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi, kuelekea katika mchezo huo dhidi ya Zalan, Nabi alisema: “Lazima kutakuwa na mabadiliko ya wachezaji watakaoanza katika kikosi chetu tofauti na wale ambao niliwatumia katika mchezo uliopita dhidi ya Azam FC na hiyo ni kutokana na sababu maalum ambazo zinapelekea haya kutokea.

 

“Katika mchezo dhidi ya Azam FC kuna sababu nyingi ambazo zilipelekea timu kubadilika, wengine walikuwa bado hawajawa fiti na wengine walitoka katika kambi ya timu ya taifa, hivyo kuelekea katika mchezo huu tutapanga wachezaji kulingana na hali zao na hapo ndipo utakapoona mabadiliko ya kikosi kilichozoeleka kubadilika,” alisema kocha huyo.

STORI: MARCO MZUMBE

Leave a Comment