
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Awali alikuwa Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam
Mhandisi Othman Sharif Khatib ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akichukua nafasi Dkt. Jones Kilembe ambaye Uteuzi wake umetenguliwa.
Dkt. David Nkanda Manyanza ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)
Hawa Abdulrahman Ghasia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo. Sylvester Jospeh Kainda ameteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya
Rufani.
