×

Simba Yafuzu Hatua ya Kwanza Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Moses Phiri akiwa katika ubora wake

KLABU ya Simba Imefuzu kwa raundi ya kwanza ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 leo Septemba 18, 2022 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.

Magoli yote ya Mnyama yamewekwa kimiani na mshambuliaji wa Zambia Moses Phiri akifunga dakika ya 29 kipindi cha kwanza na akarudi kambani kwa goli la pili dakika ya 59.

Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la pili dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi

 

Katika mchezo wa awali Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo uliopigwa Malawi hivyo Simba kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-0.

 

 

Simba itavaana na Primeiro  De Agosto ya Angola mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa tareh 8 Oktoba huku Simba ikianzia ugenini.

Leave a Comment