×

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele Awatuliza Mashabiki Atoa Ahadi ya Kibabe

Mshabuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele akifanya yake kwenye mechi yao dhidi ya Al Hilal Uwnja wa Mkapa.

 

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kwani bado wanayo nafasi nzuri ya kufanya vizuri wakiwa ugenini.

 

Yanga wameshindwa kutamba katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Hilal kutoka Sudan.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele alisema kuwa, bado safari ya kwenda makundi haijamalizika kwani wanao uwezo wa kusonga mbele wakiwa ugenini huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa moyo wa kupambana.

 

“Mashabiki tunajua jinsi gani walivyoumizwa na matokeo ya sare tukiwa nyumbani, na kwa kiasi kikubwa tunafahamu kuwa haikuwa matarajio yetu kupata sare.

 

“Tunawahakikishia mashabiki wetu kuwa tutapambana katika mchezo ujao ambao tutakuwa ugenini kuhakikisha kuwa tunaibuka na matokeo, tunawaomba mashabiki wasitukatie tamaa,” alisema mshambuliaji huyo.

Stori na Marco Mzumbe

AHMED ALLY AUNGURUMA KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI ya DE AGOSTO – “MSIMU ULIOPITA YALITUKUTA”

Leave a Comment