×

Man United Yaungana na Chelsea katika Vita ya Kumsajili Winga wa AC Milan

Mshambuliaji wa AC Milan na Timu ya Taifa ya Ureno Rafael Leao

KLABU za Manchester United pamoja na Chelsea zimeingia katika vita nzito ya kuwania Saini ya winga wa AC Milan na timu ya Taifa ya Ureno Rafael Leao.

 

Leao ambaye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Italia Serie A msimu uliopita, amebakisha miezi 18 katika mkataba wake aliona kwa sasa na mabingwa watetezi wa Ligi hiyo AC Milan.

 

Taarifa kutoka katika viunga vya Milan zinabainisha kuwa Leao amegoma kuongeza mkataba mpya wa miaka mitano aliopewa na uongozi wa AC Milan ikiwa huku akiwa ameleekeza jicho lake katika kutimka klabuni hapo.

Chelsea na Manchester United zote zinapigana vikumbo kuwania saini ya Rafael Leao

Kwa muda mrefu klabu ya Chelsea imekuwa ikihusishwa na dili la kumsajili Leao ambapo taarifa zinadai kuwa Chelsea iliulizia huduma yaw inga huyo katika majira ya kiangazi ya usajili lakini AC Milan ikatia ngumu kuwa mchezaji huyo hauzwi.

 

Chelsea pamoja na Man United zote zinatarajiwa kurejea na ofa mpya majira ya dirisha kubwa la uhamisho la kiangazi ili kuweza kupata Saini yaw inga huyo mwenye kasi na ubunifu mkubwa.

Leave a Comment