×

Netflix Imeanza Kurudisha Wafuasi Wake Baada ya Kuwapoteza Mwanzoni mwa Mwaka Huu

Kampuni ya Netflix imeanza kuwarudisha wafuasi wake baada ya kuwapoteza hapo awali

FILAMU kama Stranger Things na Monster: The Jeffrey Dahmer Story zimeisaidia kampuni ya Netflix kuweza kurudisha wasajili wake kwa kuwa filamu hizi zimefanya vizuri na kuweza kutazamwa na watu wengi duniani, Netflix wamesema katika kipindi cha Julai na Septemba imeweza kuingiza wafuasi millioni 2.4 na kuepelekea kubadilisha matokeo ya kupoteza wateja mwanzoni mwa mwaka baada ya kupandisha bei kwenye soko kuu.

 

Kwa sasa wameacha kupoteza wateja kama ilivyo kuwa hapo awali na kampuni hiyo imesema pia kuwa inatarajia kuendelea kuongeza wafuasi miezi ijayo na watapunguza bei za matumizi ya chombo hicho cha kutazama filamu pamoja na matangazo yake

 

Mashtaka mapya yanayowahusu wale watu wanaochangia akaunti moja yameanza kufanyiwa majaribio huko Marekani kwa walatino na kufikia mwaka 2025 itaanza kufanyiwa kazi mashtaka hayo kwa watumiaji wengine pia.

 

Kampuni hiyo imetengeneza njia ya kutuma profaili ya mtumiaji, historia yake ya vitu anavyovitazama na vitu anavyovipenda kwenye akaunti yake mpya na Netflix ili mipangilio binafsi ya mtumiaji isipotee.

 

Mabadiliko hayo yanaweza kuisaidia kampuni hio kutengeza pesa nyingi.

Moja ya Filamu maarufu zilizopo chini ya Kampuni ya Netflix

Kampuni ya Netflix inapitia ushindani mkubwa na makampuni mengine kama vile Amazon Prime, Apple Tv, Hulu na HBO ambazo pia zinafanya vizuri katika soko la huduma za utiririshaji wa filamu. ingawa watendaji wa kampuni ya Netflix wamekuwa mbele kusema kuwa bado wapo mbele ya mashindano katika jinsi ya kuunda filamu na kupata faida.

 

Watendaji hawa wamenukuliwa wakisema:

 

” Ni ngumu kujenga biashara kubwa na yenye faida ya utiririshaji wa filamu makisio yetu bora ni kwamba hawa washindani wengine wanapoteza hela kwenye utiririshaji wa filamu.”

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment