×

Msanii Takeoff wa Kundi Maarufu la Migos Auawa kwa Kupigwa Risasi Kichwani

 

MSANII wa kundi la Migos kutoka nchini Marekani, Takeoff ameuawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya leo, tukio lililotokea katika viwanja vya michezo vya 810 Billiards & Bowling, Houston huku memba mwingine wa kundi hilo, Quavo akinusurika.

 

Taarifa zinaeleza kwamba, Takeoff na mwenzake Quavo, walikuwa wakicheza mchezo wa Dice pamoja na marafiki zao ambapo katika mazingira ambayo bado hayaeleweki, kulitokea mabishano kati yao na kundi la vijana wengine waliokuwa eneo hilo, kisha milio ya risasi ikasikika.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda, risasi iliyofyatuliwa, ilimpiga Takeoff kichwani na kusababisha apoteze maisha papo hapo, huku Quavo akionekana akijaribu kumsaidia memba mwenzake huyo wa Migos kuokoa maisha yake ingawa tayari alikuwa amechelewa.

 

Taarifa za awali kutoka kwa Polisi wa Houston, zinaeleza kuwa watu wengine wawili walijeruhiwa kwa risasi katika tukio hilo na uchunguzi unaendelea.

 

Saa chache kabla ya tukio hilo, Takeoff aliposti picha mtandaoni akiwa katika uwanja huo, akifurahi na marafiki zake, ikiwa ni baada ya usiku wa jana, kukesha kwenye ‘bethidei’ ya rafiki yao, Jas Prince.

 

Leave a Comment