×

Padri Avamiwa na Watu Wenye Silaha na Kuchomwa Moto Hadi Kufa Nchini Nigeria

Padri Isaac Aichi aliyevamiwa na kuchomwa moto hadi kufana watu wenye silaha nchini Nigeria.

 

Padri wa Kanisa Katoliki nchini Nigeria, Isaac Achi amefariki dunia kwa kuungua na moto baada ya watu wasiojulikana kushambulia makazi yake kisha kuchoma moto nyumba aliyokuwa anaishi, tukio lililotokea jana Jumapili, Januari 15, 2023.

Padri Aichi, alikuwa kiongozi wa kanisa la Mtakatifu Petro na Paulo lililopo katika Mji wa Kafin-Koro katika Jimbo la Niger State ambapo msemaji wa polisi, ameeleza kuwa msaidizi wake, Collins Omeh alipigwa risasi wakati akijaribu kukimbia.

Msemaji wa Polisi katika jimbo hilo, Wasiu Abiodun amenukuliwa akisema kuwa watu wenye silaha, walijaribu kuingia ndani ya nyumba ya padri huyo lakini walishindwa ndipo walipoamua kuichoma moto nyumba hiyo, padri akiwa ndani.

Ameeleza kuwa baada ya polisi kupata taarifa hizo, walifika eneo la tukio lakini tayari padri huyo alikuwa amefariki dunia kwa kuungua huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.

Leave a Comment