×

BoT Yaongeza Miamala Mtandaoni, Yashusha Riba ya Benki

Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania imepitisha hatua mbalimbali za kisera zinazolenga kukabiliana na athari za mlipuko wa #COVID19 katika Uchumi ili kudumisha uthabiti wa Sera ya fedha.

1. Kampuni zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya mtandao kuongeza kiwango cha miamala kwa siku kwa mteja kutoka Tsh. Milioni 3 hadi Tsh. Milioni 5 na kiwango cha akiba kwa siku cha mteja kutoka Tsh. Milioni 5 hadi Tsh. Milioni 10.

2. Kuongeza unafuu kwenye dhamana na hati fungani za Serikali zinanazotumika na benki kama dhamana wakati wa kukopa Benki Kuu. Kiwango cha dhamana kimepunguzwa kutoka 10% hadi 5% kwa dhamana za muda mfupi na pia kutoka 40% hadi 20% kwa hati fungani.

3. Benki Kuu itatoa unafuu kwa benki na taasisi za fedha zitakazotoa unafuu katika kurejeshwaji wa mikopo kwa namna zinavyoona inafaa na kujadiliana na Wakopaji kwa kuzingatia uwazi bila upendeleo.

 

4. Imeshusha kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania, kutoka asilimia 7 hadi asilimia 6. Pia, imeshusha kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa kutoka 7% hadi 5%.

Aidha, Benki Kuu inaufahamisha Umma kuwa nchi yetu ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kuwezesha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi na Wananchi wanahimizwa kufanya miamala kwa kutumia Shilingi badala ya fedha za kigeni.

Leave a Comment