
Mchezaji soka wa Ghana aliyewahi kuichezea Klabu ya Chelsea, Christian Atsu amefariki dunia na mwili wake kukutwa ukiwa umefukiwa kwenye kifusi kufuatia tetemeko kubwa lililotokea wiki iliyopita nchini Uturuki.
Taarifa zilizothibitishwa na wakala wa mchezaji huyo, Murat Uzunmehmet zimeeleza kuwa Atsu ambaye alikuwa miongoni mwa maelfu ya watu waliofukiwa na kifusi kutokana na tetemeko hilo, amekutwa kwenye kifusi kwenye makazi yake, Kusini mwa Uturuki.

Mpaka anafikwa na mauti, Atsu alikuwa akiichezea Klabu ya Hatayspor ya nchini Uturuki ambapo mara ya mwisho, alicheza mechi ya Ligi Kuu ya Uturuki, Super Lig Februari 5, 2023 ambapo alifunga.
Murat amenukuliwa akisema simu ya Atsu pamoja na vifaa vyake vingine vimepatikana.