×

Polisi wamsaka mrembo

juliana2Juliana Elias akiwa na mtoto wake kabla ya kumtelekeza.

DAR ES SALAAM: Mrembo Juliana Elias Komba (18), anasakwa na Jeshi la Polisi Kimara kwa hati ya utambulisho KMR/RB/12841/2015 kosa likidaiwa kumtelekeza mwanaye, Jordan Gwamaka (1).

Akizungumza na mwandishi wetu, Januari 11, mwaka huu kwenye ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar, mama mzazi wa binti huyo, Lillian David Mwambungu alisema amelazimika kulivalia njuga suala hilo na kuhakikisha binti yake anakamatwa kwani amefanya kitendo cha kinyama ambacho hakivumiliki.

“Nimefikia hatua ya kwenda kuripoti polisi si kwamba simpendi mwanangu, nafanya hivi ili kumuepushia tabia hii mbaya ya kumuacha mtoto mdogo ambaye ni mgonjwa huku mwenyewe akienda mtaani kufanya madudu. Huyu mtoto alizaliwa akiwa na tatizo la uvimbe kichwani, baadaye akagundulika ana henia.

“Wakati anajifungua, Juli mwenyewe alipata tatizo la kifafa cha uzazi, nilimhudumia kwa msaada wa madaktari akapona. Kinachoniumiza baada ya kupona, nilimtafuta daktari akanisaidia kumfanyia upasuaji mtoto, ambapo aliwekewa mpira kichwani hivyo tukashauriwa kuwa karibu naye na Juli ndiye alikuwa akishinda naye wakati mimi natafuta fedha ya kula.

“Juli amefanya jambo la kinyama sana kumuacha mwanaye chumbani tena akimfungia wakati anajua wazi ni mgonjwa na mimi nimepigania maisha yake.

“Mimi nilikuwa nikiambiwa na majirani tu kwamba, mtoto anaachwa peke yake. Siku nyingine anamnywesha dawa za usingizi (valium), yeye anakwenda kuzurura. Mwishoni mwa mwaka jana alitokomea kusikojulikana wakati mtoto wake anatakiwa kufanyiwa upasuaji mwingine,” alisema mama huyo.

Alisema anaomba yeyote atakayemwona Juliana (angalia picha Uk.16), atoe taarifa kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye ili aweze kukamatwa.

Leave a Comment