Wizara ya Afya imepokea taarifa ya kuwepo Ugonjwa huo katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangereko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega ambapo Watu 7 walipata dalili za Ugonjwa na Watano (5) wamefariki dunia
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Watu hao walipata dalili za Homa, Kutapika, Kutokwa Damu sehemu mbalimbali za Mwili na Figo kushindwa kufanya kazi na hadi sasa Wagonjwa 2 wako Hospitali
Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa Ugonjwa na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae