×

Mayele, Aziz Ki Waongeza Mzuka Yanga leo Jumapili dhidi ya TP Mazembe

Mshambuliaji wa Yanga Fiston kalala mayele.

KUELEKEA mchezo wao wa leo Jumapili dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kupigwa nchini DR Congo, uongozi wa Yanga umetamba kuwa tayari kikosi chao kimekamilika na wachezaji wote waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa wamewasili kwa ajili ya kumaliza kazi leo.

Yanga leo Jumapili wanatarajiwa kuwa wageni wa TP Mazembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa nchini DR Congo, ambapo Yanga wataingia wakiwa vinara wa msimamo na pointi zao 10.

Aziz Ki

Mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba ya kundi D la mashindano kwani tayari Yanga wameshafanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali. Kwa wachezaji waliojiunga na Yanga DR Congo Musonda ndiye alikuwa wa kwanza kuripoti kambini kabla ya Mayele na Aziz Ki ambao walifika Jumamosi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema: “Baada ya kuwasili hapa DR Congo kikosi chetu kimeendelea na programu za maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe tunatarajia mchezo mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wetu hasa wanapocheza nyumbani.

“Wachezaji wote waliosalia ambao walikuwa na majukumu ya timu ya Taifa tayari wamejiunga na timu na baadhi wanatarajiwa kujiunga leo (jana) Jumamosi wakiwemo Mayele Fiston na Aziz Ki Stephanie.”

STORI NA JOEL THOMAS

YANGA WAFICHUA SIRI ya KUSAFIRI na TAJIRI GSM KWENDA CONGO, WAITAJA DABI ya KARIAKOO…

Leave a Comment